Zaburi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziJina la kitabu hiki kwa Kiebrania ni “Sepher Tehillim”, ambalo maana yake ni “Nyimbo za Sifa.” Jina la Kiyunani ni “Psalmoi” yaani “Nyimbo zinazoimbwa kwa kutumia ala za muziki za nyuzi” na ndiyo kiini cha kitabu hiki. Kitabu hiki kina sura mia moja na hamsini, na sura nyingi zinajitosheleza, isipokuwa chache tu. Zaburi ya mwisho (150) ni wimbo wa sifa, kuonesha kuwa kilele cha kitabu kizima ni wimbo wa sifa.Zaburi zilitungwa kwa mvuto wa hali ya juu na wa kusisimua sana na hivyo huwa zinaleta msisimko wa pekee. Kwa kuwa zilitungwa kutokana na uzoefu wa maisha kutoka mazingira na nyakati mbalimbali, bado zimekuwa na mvuto mkubwa ulimwenguni kote kwa miaka mingi tangu ziandikwe.Mara kwa mara, Zaburi zimeainishwa kwa kufuata namna fulani za maelezeo au mafundisho. Aina mbalimbali za zaburi hizo ni kama vile zile zilizohusu sala ya shukrani na sifa, maombolezo, nyimbo za kuonesha tumaini kwa Mwenyezi Mungu, toba, kusimika au kutawaza viongozi, kuhusu Masihi, historia ya uumbaji, na zilizohusu hekima ya jinsi binadamu anavyopaswa kutunza mahusiano mema na Mwenyezi Mungu na jirani yake.Inaaminika kwamba makusanyo ya awali yalifanywa na Daudi. Nyongeza nyingine na mpangilio inawezekana vilifanywa na Sulemani, Yehoshafati, Hezekia, Yosia na wengine.WaandishiInaaminiwa kuwa kitabu cha Zaburi ni matokeo ya kazi ya watu wengi, wakiwemo: Daudi (73), Asafu (12), Wana wa Kora (10), Musa (1), Hemani (1), Ethani (1), na Sulemani (2). Waandishi wa Zaburi hamsini hawajulikani.KusudiKuelezea umuhimu wa mashairi katika sifa, kuabudu na kukiri dhambi mbele za Mwenyezi Mungu.MahaliPalestina na Babeli.TareheKati ya wakati wa Musa (1440 K.K.) na wakati wa utumwa wa Babeli (586 K.K.).Wahusika WakuuDaudi, Asafu, Wana wa Kora, Musa, Hemani na Sulemani.Wazo KuuKusifu ni kutambua na kutangaza ukuu wa Mwenyezi Mungu, kufurahia na kudhihirisha wema wake.Mambo MuhimuZaburi zimeelezea ufunuo wa Mwenyezi Mungu, uumbaji, hali ya mwanadamu, wokovu, dhambi na uovu, toba, haki na uadilifu, kuabudu na kusifu, maombi na hukumu.YaliyomoKitabu cha kwanza: 1–41Kitabu cha pili: 42–72Kitabu cha tatu: 73–89Kitabu cha nne: 90–106Kitabu cha tano: 107–150.