Wimbo Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziKitabu hiki kinaitwa “Wimbo Ulio Bora,” yaani “Wimbo Mzuri kupita Nyimbo Zote.” Hii ni tafsiri ya moja kwa moja kutoka maneno ya Kiebrania, “Shir Hash-Shirim,” na kwa Kiyunani “Asma Asmaton.” Hili ndilo chimbuko la jina linalokitambulisha kitabu hiki.MwandishiSulemani.KusudiKuthibitisha utakatifu wa Mwenyezi Mungu, furaha, heshima na upendo katika ndoa kulingana na kusudi la Mwenyezi Mungu, na kudhihirisha upendo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake.MahaliBustani ya mwanamke Mshulami na jumba la kifalme.TareheInadhaniwa kuwa miaka ya mwanzo ya utawala wa Sulemani.Wahusika WakuuMfalme Sulemani, Mwanamke Mshulami, na rafiki zao.Wazo KuuUpendo wa dhati kati ya mume na mke katika ndoa.Mambo MuhimuMambo yanayohusu upendo na ndoa.YaliyomoBibi arusi na bwana arusi (1:1–2:7)Sifa za mpenzi wake (2:8–3:5)Kumsifu bibi arusi (3:6–5:1)Upendo wenye msukosuko (5:2–7:9)Urafiki ambao haujavunjika (7:10–8:14).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help