Yoeli Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziYoeli mwana wa Pethueli maana ya jina lake ni “Mwenyezi Mungu ni Mwenyezi Mungu”. Nyingi ya kumbukumbu zake katika kitabu hiki na huduma yake hekaluni zinaonesha kwamba alikuwa nabii aliyetumwa kwa Yuda na Yerusalemu. Kutokana na huduma yake, wengi wamemdhania kuwa nabii wa “kikuhani” (linganisha Yeremia 28:1, 5) aliyenena neno la kweli la Bwana.Tukio hili lilitafsiriwa kuwa ni pigo kwa sababu ya dhambi za watu. Yoeli alilitafsiri tukio hili kuwa ni kielelezo cha ujio wa “siku ya Mwenyezi Mungu”, yaani siku ya hukumu. Tukio hili la nzige lilileta maombolezo makubwa katika nchi ya Palestina na kupelekea makuhani kulia kilio kikuu. Hata hivyo, kitabu kinaonesha kuwa tukio la nzige halikuwa neno la mwisho kwani baada ya maombolezo makubwa, watu walifarijiwa kwa kuahidiwa kupata furaha kuu. Akiwaonya watu wamgeukie Mwenyezi Mungu kwa toba, Yoeli anatangaza kwamba “siku ya Mwenyezi Mungu” inakuja kwa ajili ya hukumu. Lakini Yoeli anaonesha kuwa kabla siku ya hukumu haijatimia, Mwenyezi Mungu atatuma Roho wake Mtakatifu ili kuleta baraka. Katika tukio la nzige, Yoeli aliona ishara ya hukumu ya mwisho, hivyo akawaonya watu watubu na kumrudia Mwenyezi Mungu.MwandishiYoeli mwana wa Pethueli.KusudiKuonya Yuda juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa karibu kwa sababu ya dhambi zake; na kuwahimiza watu wamrudie Mwenyezi Mungu.MahaliYerusalemu.TareheMnamo 835–796 K.K.Wahusika WakuuYoeli na watu wa Yuda.Wazo KuuHukumu na kumrudia Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuPigo la nzige, kuwaonya watu watubu, na tumaini kwa watu wa Mwenyezi Mungu.YaliyomoKuvamiwa na nzige (1:1–2:17)Maonyo na baraka za Mwenyezi Mungu (2:18–3:12).