3 Yohana Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziWaraka wa tatu wa Yohana uliandikiwa Gayo, ambaye alikuwa kiongozi muhimu katika fulani. Alielekezwa kuwasaidia na kuwahudumia wajumbe wa Mwenyezi Mungu waliotembelea kundi la waumini. Pia alipewa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano. Yohana alieleza tarajio lake la kuja na kushughulikia tatizo hili mwenyewe.MwandishiMtume Yohana.KusudiYohana anamwandikia Gayo akimpa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano.MahaliEfeso.TareheMnamo 90 B.K.Wahusika WakuuYohana, Gayo, Deotrefe, na Demetrio.Wazo KuuWajibu binafsi wa Gayo kuhusu watumishi wa kweli na wa uongo.Mambo MuhimuYohana anamtakia Gayo kufanikiwa katika mambo yote, na pia anamwagiza asiige lililo baya bali aige lililo jema.YaliyomoSalamu (1-4)Gayo anatiwa moyo (5-8)Deotrefe anakemewa (9-10)Demetrio anasifiwa (11-12)Hitimisho (13-15).