Zaburi 133 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 133Sifa za pendo la unduguWimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza

ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,

yakitiririka kwenye ndevu,

yakitiririka kwenye ndevu za Haruni,

hadi kwenye upindo wa mavazi yake.

3Ni kama umande wa Hermoni

ukianguka juu ya Mlima Sayuni.

Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake,

naam, uzima hata milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help