Zekaria Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziMaana ya jina Zekaria ni “Mwenyezi Mungu amekumbuka”. Zekaria alikuwa kijana wakati alipoanza huduma yake. Zekaria aliwaonya watu waliokuwa wameanza kujenga upya Hekalu kwamba iliwapasa kusikiliza ujumbe wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa manabii. Aliwahimiza kudumisha uhusiano na Mwenyezi Mungu ili wasiiharakishe hukumu ya Mwenyezi Mungu. Maono ya nabii Zekaria yalikuwa ya kuwatia moyo wajenzi katika wakati mgumu, na kuwahakikishia kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa na mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.Sehemu ya mwisho ya huduma yake, Zekaria alikazia mpango wa maendeleo wa muda mrefu, akionesha kuanzishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa unyenyekevu akileta wokovu, lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe, yaani Waisraeli. Mataifa yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisraeli watamtambua Masihi na wataibuka na ushindi, nayo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme.MwandishiZekaria.KusudiKuwatia moyo Waisraeli na kuwajulisha mpango wa Mungu wa baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masihi.MahaliYerusalemu.TareheSura 1–8: mnamo 520–518 K.K.; sura 9–14: mnamo 480–470 K.K.Wahusika WakuuZekaria, Zerubabeli, Yoshua na Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni.Wazo KuuAhadi za Masihi na kumalizia ujenzi wa Hekalu.Mambo MuhimuZekaria alieleza juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya adui za Israeli, baraka kwa ajili ya Yerusalemu, na umuhimu wa watu wa Mwenyezi Mungu kudumu katika utakatifu. Mwenyezi Mungu atawahukumu adui wa Israeli, na Mfalme (yaani Masihi) atakuja.YaliyomoUtangulizi (1:1-6)Maono nane ya kinabii (1:7–6:8)Kutawazwa kwa Yoshua kinabii (6:9-15)Jumbe mbalimbali za hukumu na matumaini (7:1–11:3)Kuja kwa Masihi na kukataliwa kwake (11:4–13:9)Mwenyezi Mungu yuaja kutawala (14:1-21).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help