Obadia Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziJina Obadia lina maana ya “Mtumishi wa Yehova.” Habari za nabii Obadia hazipatikani popote nje ya kitabu hiki. Unabii wa kitabu hiki unahusu hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya taifa la Edomu, na kukomeshwa na kuangamizwa kwa taifa hilo kwa sababu ya kiburi na udhalimu wake. Waedomu, waliokuwa uzao wa Esau, walijivunia usalama katika ngome zao kwenye Mlima Seiri, kusini mwa Bahari ya Chumvi. Askari wao walitumika katika jeshi la Nebukadneza baada ya Yerusalemu kutekwa na kuteketezwa mnamo 587 K.K. Waedomu waliwadharau watu wa Yuda, na hawakuwasaidia walipopatwa na mikasa ya kuvamiwa na kupigwa na majeshi ya kigeni. Mwanzoni mwa karne ya tisa, Waedomu wenyewe walishiriki zaidi ya mara nne kuiteka Yerusalemu.MwandishiObadia.KusudiKudhihirisha hasira kuu ya Mwenyezi Mungu na hukumu yake dhidi ya Waedomu.MahaliYerusalemu.TareheInadhaniwa kuwa mnamo 605–586 K.K.Wahusika WakuuWaedomu.Wazo KuuHukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Waedomu.Mambo MuhimuDharau, kiburi na udhalimu wa Waedomu na hukumu ya Mwenyezi Mungu kwao.YaliyomoMaangamizi ya Edomu (1-14)Kurejeshwa kwa Israeli (15-21).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help