Zaburi 114 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 114Maajabu ya Mwenyezi Mungu wakati Israeli walitoka Misri

1Israeli alipotoka Misri,

nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,

2Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu,

Israeli akawa milki yake.

3Bahari ilitazama ikakimbia,

Yordani ulirudi nyuma,

4milima ilirukaruka kama kondoo dume,

vilima kama wana-kondoo.

5Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,

nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,

6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume,

enyi vilima, kama wana-kondoo?

7Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,

mbele za Mungu wa Yakobo,

8aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,

mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help