Zaburi 14 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 14Uovu wa wanadamu(Zaburi 53)Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Mpumbavu anasema moyoni mwake,

“Hakuna Mungu.”

Wamepotoka, matendo yao ni maovu kabisa;

hakuna hata mmoja atendaye mema.

2Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamu

kutoka mbinguni

aone kama kuna mwenye hekima,

yeyote anayemtafuta Mungu.

3Wote wamepotoka,

wote wameoza pamoja;

hakuna atendaye mema,

naam, hakuna hata mmoja!

4Je, watendao maovu kamwe hawatajifunza:

wale ambao huwala watu wangu

kama watu walavyo mkate,

hao ambao hawamwiti Mwenyezi Mungu?

5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,

maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.

6Ninyi watenda maovu mnakwamisha mipango ya maskini,

bali Mwenyezi Mungu ndiye kimbilio lao.

7Laiti wokovu wa Israeli

ungekuja kutoka Sayuni!

Mwenyezi Mungu anaporejesha

wafungwa wa watu wake,

Yakobo na ashangilie,

Israeli na afurahi!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help