Zaburi 99 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 99Mwenyezi Mungu Mfalme mtakatifu

1Mwenyezi Mungu anatawala,

mataifa na yatetemeke;

anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,

dunia na itikisike.

2Mwenyezi Mungu ni mkuu katika Sayuni;

ametukuzwa juu ya mataifa yote.

3Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:

yeye ni mtakatifu!

4Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,

wewe umethibitisha adili;

katika Yakobo umefanya

yaliyo haki na sawa.

5Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;

yeye ni mtakatifu.

6Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,

Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;

walimwita Mwenyezi Mungu,

naye aliwajibu.

7Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;

walizishika sheria zake na amri alizowapa.

8Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

ndiwe uliyewajibu,

kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,

ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

9Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,

mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,

kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help