Amosi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziAmosi maana yake ni “Mchukua mzigo”. Yeye alikuwa mchunga wanyama na pia mtunza mikuyu kutoka Tekoa, kijiji kilichokuwa karibu na Bethlehemu na kilomita 16 kutoka Yerusalemu. Mwenyezi Mungu alimwita kuwa nabii katika Ufalme wa Kaskazini (Israeli) na alifanya kazi wakati mmoja na nabii Hosea. Wakati huo ufalme ulikuwa na utajiri mwingi. Ujumbe wa Amosi unaonesha kwamba wakati huo ulikuwa wa mafanikio mengi kiuchumi na kisiasa katika Israeli kuliko nyakati zingine zote, isipokuwa zile za enzi ya Sulemani.Hata hivyo, Amosi aliona uovu na ubatili mwingi katika miji ya Yuda iliyokuwa katika ufalme wa kaskazini. Watu wengi waliishi katika dimbwi la umaskini wakati matajiri waliishi maisha ya anasa na ya kifahari. Rushwa, ukosefu wa haki, na manyanyaso ya matajiri na wenye nguvu dhidi ya watu wanyonge vilikithiri. Kwa jumla, miji ilitawaliwa na uovu na haikuwa na uchaji kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, katika unabii wake, Amosi alikemea vikali hali hii na aliwaonya watu wamrudie Mwenyezi Mungu.MwandishiAmosi.KusudiKukemea matendo maovu, kukosekana kwa uadilifu na kutangaza hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya watendao maovu hayo; kuwahimiza watu kutenda haki na kufanya ibada za kweli mbele za Mwenyezi Mungu.MahaliSamaria, Betheli, Gilgali.TareheMnamo 760–755 K.K.Wahusika WakuuAmosi, Amazia, na Yeroboamu wa Pili.Wazo KuuHaki, uadilifu na hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya dhambi.Mambo MuhimuAmosi ametumia mifano ya maneno ya kusisimua kutokana na uzoefu wake wa ukulima na uchungaji wa wanyama: simba angurumaye, kipande cha kondoo kilichopokonywa kinywani mwa simba, ng’ombe walioshiba, kapu la matunda, na mifano mingine.YaliyomoHukumu kwa Israeli na mataifa jirani (1:1–2:16)Uovu wa Israeli (3:1–6:14)Maono matano (7:1–9:10)Kurejeshwa kwa Israeli (9:11-15).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help