Zaburi 126 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 126Kurejeshwa kutoka uhamishoWimbo wa kwenda juu.

1Mwenyezi Mungu alipowarejesha mateka Sayuni,

tulikuwa kama watu walioota ndoto.

2Vinywa vyetu vilijaa kicheko,

ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.

Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,

“Mwenyezi Mungu amewatendea mambo makuu.”

3Mwenyezi Mungu ametutendea mambo makuu,

nasi tumejaa furaha.

4Ee Mwenyezi Mungu, turejeshee watu wetu waliotekwa,

kama vijito katika Negebu.

5Wapandao kwa machozi

watavuna kwa nyimbo za shangwe.

6Yeye azichukuaye mbegu zake

kwenda kupanda, huku akilia,

atarudi kwa nyimbo za shangwe,

akichukua miganda ya mavuno yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help