Zaburi 125 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 125Usalama wa watu wa Mwenyezi MunguWimbo wa kwenda juu.

1Wale wamtumainio Mwenyezi Mungu ni kama Mlima Sayuni,

ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.

2Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,

ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowazunguka watu wake

sasa na hata milele.

3Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi

waliyopewa wenye haki,

ili wenye haki wasije wakatumia

mikono yao kutenda ubaya.

4Ee Mwenyezi Mungu, watendee mema walio wema,

wale walio wanyofu wa moyo.

5Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,

Mwenyezi Mungu atawafukuza pamoja na watenda maovu.

Amani iwe juu ya Israeli.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help