Zaburi 93 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 93Mwenyezi Mungu ni mkuu

1Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu;

Mwenyezi Mungu amejivika utukufu

tena amejivika nguvu.

Dunia imewekwa imara,

haitaondoshwa.

2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;

wewe umekuwa tangu milele.

3Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu,

bahari zimepaza sauti zake;

bahari zimepaza sauti za mawimbi yake.

4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,

ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:

Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu.

5Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara;

utakatifu umepamba nyumba yako

pasipo mwisho.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help