Zaburi 3 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 3Sala ya asubuhi ya kuomba msaadaZaburi ya Daudi. Alipomkimbia mwanawe Absalomu.

1Ee Mwenyezi Mungu, tazama adui zangu walivyo wengi!

Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

2Wengi wanasema juu yangu,

“Mungu hatamwokoa.”

3Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote;

umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

4Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu,

naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.

5Ninajilaza na kupata usingizi;

naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza.

6Sitaogopa makumi elfu ya adui,

wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

7Ee Mwenyezi Mungu, amka!

Niokoe, Ee Mungu wangu!

Wapige adui zangu wote kwenye taya,

vunja meno ya waovu.

8Kwa maana wokovu watoka kwa Mwenyezi Mungu.

Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help