Zaburi 127 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 127Bila Mwenyezi Mungu, kazi ya mwanadamu haifaiWimbo wa kwenda juu. Wa Sulemani.

1Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba,

wajengao hufanya kazi bure.

Mwenyezi Mungu asipoulinda mji,

walinzi wakesha bure.

2Mnajisumbua bure kuamka mapema

na kuchelewa kulala,

mkitaabikia chakula:

kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake.

3Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,

uzao ni zawadi kutoka kwake.

4Kama mishale mikononi mwa shujaa

ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

5Heri mtu ambaye podo lake

limejazwa nao.

Hawataaibishwa wanaposhindana

na adui zao langoni.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help