Sefania Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziJina “Sefania” maana yake ni “Aliyefichwa na Yehova”. Sefania alikuwa wa ukoo wa Hezekia, mfalme wa Yuda. Nabii Sefania alihudumu wakati wa utawala wa Mfalme Yosia (mwaka 636–609 K.K). Sefania alionya kwamba siku ya Bwana ingeleta hukumu kwa Yuda pamoja na Yerusalemu, hivyo akawashauri Wayahudi kumrudia Mwenyezi Mungu. Uvamizi wa kuteka Yuda ulikuwa unakuja kutoka kaskazini, nao ungeyakumba pia mataifa yaliyowazunguka. Ingawa hukumu ya Yuda imeainishwa, ahadi ya kufanywa upya ni yakini. Mataifa yatahukumiwa na kutiishwa na mfalme wa Israeli, atakayetawala kutoka Sayuni.MwandishiSefania.KusudiKuwaonya watu wa Yuda kuacha ibada ya sanamu na maovu yote na kumrudia Mwenyezi Mungu.MahaliYerusalemu.TareheMnamo 640–609 K.K.Wahusika WakuuSefania, na watu wa Yuda.Wazo KuuSefania aliwapa watu matumaini kwamba Mwenyezi Mungu angewarudisha watu wake nyumbani.Mambo MuhimuHukumu na urejesho kwa watu wa Yuda.YaliyomoKutangazwa kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu (1:1–2:3)Hukumu dhidi ya mataifa (2:4-15)Maisha ya baadaye ya Yerusalemu (3:1-20).