Waefeso Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziPaulo aliandika waraka huu akiwa gerezani huko Rumi ili kuwatia moyo waumini wa jimbo la Asia. Waraka huu ulikuwa kama mwongozo uliokusudiwa kwa makundi kadhaa ya waumini wa Isa Al-Masihi. Zaidi ya hayo, kwenye waraka huu hakuna salamu za watu binafsi, wala hakuna matatizo maalum. Paulo alielezea kwamba jumuiya ya waumini ilianzishwa na Mwenyezi Mungu, akiwaelezea mpango wa Mungu wa tangu awali wa kuwaokoa watu wake kupitia Al-Masihi kwa imani. Mpango huu ulikuwako hata kabla ya ulimwengu kuumbwa. Mwenendo wa maisha mapya upo kinyume kabisa na ule wa maisha ya kale bila Al-Masihi.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuwaimarisha waumini katika imani yao ya wafuasi wa Al-Masihi kwa kueleza asili na kusudi la jumuiya ya waumini wa Isa, ambayo ni mwili wa Isa Al-Masihi.MahaliRumi.TareheMnamo 60 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Tikiko, na waumini wa Efeso.Wazo KuuMpango wa Mwenyezi Mungu wa milele wa kuuokoa ulimwengu ulitimizwa kupitia kwa Al-Masihi katika mwili wake.Mambo MuhimuUmoja katika Al-Masihi na maisha mapya katika Al-Masihi (2:4-6), na umoja katika mwili wa Al-Masihi. Pia maisha wafuasi wa Al-Masihi wanayopaswa kuishi kuhusu ndoa, tabia, mwenendo, wazazi na watoto, watumishi na mabwana zao.YaliyomoMpango wa Mwenyezi Mungu, na wokovu wa wote wanaomwamini (1:1–2:22)Siri ya Injili (3:1-21)Maisha ya mfuasi wa Al-Masihi duniani (4:1–6:9)Silaha za Mwenyezi Mungu, salamu za mwisho (6:10-24).