Zaburi 117 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
Zaburi 117Sifa za Mwenyezi Mungu
1Msifuni Mwenyezi Mungu, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
2Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa Mwenyezi Mungu unadumu milele.
Msifuni Mwenyezi Mungu.