Zaburi 43 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 43Maombi ya mtu aliye uhamishoni yanaendelea

1Ee Mungu unihukumu,

nitetee dhidi ya taifa lisilomcha Mungu,

niokoe na watu wadanganyifu na waovu.

2Wewe ni Mungu ngome yangu.

Kwa nini umenikataa?

Kwa nini niendelee kuomboleza,

nikidhulumiwa na adui?

3Tuma hima nuru yako na kweli yako viniongoze;

na vinilete hadi mlima wako mtakatifu,

mahali unapoishi.

4Ndipo nitaenda madhabahuni pa Mungu,

kwa Mungu, furaha yangu na shangwe yangu.

Nitakusifu kwa kinubi,

Ee Mungu, Mungu wangu.

5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?

Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

Weka tumaini lako kwa Mungu,

kwa sababu bado nitamsifu

Mwokozi wangu na Mungu wangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help