1Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2Unirehemu Mwenyezi Mungu,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Mwenyezi Mungu, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.
Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini?
4Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5Hakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa Kuzimu?
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha natiririsha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha kiti changu
kwa machozi yangu.
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu.
9Mwenyezi Mungu amesikia kilio changu kwa huruma,
Mwenyezi Mungu amekubali sala yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.