Zaburi 101 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 101Ahadi ya kuishi kwa uadilifu na kwa hakiZaburi ya Daudi.

1Nitaimba kuhusu upendo wako na haki yako;

kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, nitaimba sifa.

2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:

utakuja kwangu lini?

Nitatembea nyumbani mwangu

kwa moyo usio na lawama.

3Sitaweka mbele ya macho yangu

kitu kiovu.

Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;

hawatashikamana nami.

4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;

nitajitenga na kila ubaya.

5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,

huyo nitamnyamazisha;

mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi

huyo sitamvumilia.

6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,

ili waweze kuishi pamoja nami;

yeye ambaye moyo wake hauna lawama

atanitumikia.

7Mdanganyifu hatakaa

nyumbani mwangu,

yeye asemaye kwa uongo

hatasimama mbele yangu.

8Kila asubuhi nitawanyamazisha

waovu wote katika nchi;

nitamkatilia mbali kila mtenda maovu

kutoka mji wa Mwenyezi Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help