Yona Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziJina Yona maana yake ni “Hua”. Kitabu hiki kinaelezea yale yaliyomtokea Yona kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Yona alikuwa ameagizwa na Mwenyezi Mungu aende kuwaonya watu wa Ninawi juu ya hukumu iliyokuwa inakuja. Alijaribu kumkimbia Mwenyezi Mungu na kuelekea Tarshishi, upande wa magharibi wa Israeli badala ya kuelekea Ninawi iliyokuwa kaskazini mashariki. Yona alitupwa baharini akamezwa na samaki mkubwa sana ambaye alimtapika pwani ya mashariki mwa Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na kuwaonya watu kuhusu hukumu ya Mwenyezi Mungu na watu wa Ninawi walitubu. Badala ya kufurahia jambo hili, Yona alihuzunika na kuvunjika moyo kwa sababu Mwenyezi Mungu alionesha rehema na kughairi hukumu dhidi ya watu wa Ninawi.MwandishiYona mwana wa Amitai.KusudiKuonesha ukuu wa rehema za Mwenyezi Mungu na wokovu kwa mwanadamu. Pia, kuonesha jinsi ambavyo mwanadamu hawezi kukimbia wito wa Mwenyezi Mungu.MahaliInaweza kuwa Israeli au Ninawi.TareheInadhaniwa kuwa mnamo 785–760 K.K.Wahusika WakuuYona, nahodha wa meli na mabaharia, mfalme wa Ninawi, na Waninawi wote.Wazo KuuUkuu wa rehema za Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuRehema za Mwenyezi Mungu na upendo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote.YaliyomoYona amkimbia Mwenyezi Mungu (1:1-17)Maombi ya Yona na kuokolewa (2:1-10).Yona aenda Ninawi (3:1-10)Hasira ya Yona kwa ajili ya huruma ya Mwenyezi Mungu (4:1-11).