Wafilipi Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziPaulo alitembelea mji wa Filipi katika safari yake ya pili kueneza Injili, kutokana na maono aliyoyapata akiwa Troa kumwelezea aelekee Makedonia. Filipi hapakuwa na Sinagogi kwa sababu ya idadi ndogo ya Wayahudi. Waumini wa Filipi walimpelekea Paulo msaada kupitia kwa Epafrodito. Pia alitumia nafasi hiyo kuelezea matatizo aliyopata huko Rumi. Waumini wote waliambiwa wawe na malengo ya juu kabisa katika maisha yao ya wafuasi wa Al-Masihi, kwa maana Mwenyezi Mungu angewatimizia mahitaji yao yote katika maisha. Paulo aliwahimiza kufurahi nyakati zote.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuwashukuru rafiki zake wapendwa waliokuwa wamempelekea msaada kwa ajili ya mahitaji yake. Kuwatia Wafilipi moyo na kuwataka kusimama imara, akiwahimiza wawe na unyenyekevu kama aliokuwa nao Al-Masihi, na pia wawe na umoja.MahaliRumi.TareheMnamo 61 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Timotheo, Epafrodito, Euodia na Sintike.Wazo KuuPaulo alisisitiza kuhusu furaha ya muumini katika Al-Masihi.Mambo MuhimuPaulo anaagiza waumini kukataa kabisa mafundisho ya uongo na kuwahimiza wafurahi nyakati zote.YaliyomoPaulo na matatizo yake huko Rumi (1:1-30)Kumwiga Al-Masihi (2:1-30)Mafundisho kuhusu mwenendo wa mfuasi wa Al-Masihi (3:1-21)Mausia, shukrani na salamu za mwisho (4:1-23).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help