Wagalatia Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziPaulo aliandika waraka huu katika safari yake ya kwanza kueneza Injili. Baada yake kuondoka Galatia, waumini Wayahudi walifika huko, nao wakaanza kusisitiza kwamba lazima watu wa Mataifa walioamini kwanza watimize Torati ya Musa ili wapate kuokoka. Paulo aliandika kupinga mafundisho hayo, akionesha jinsi Ibrahimu, ambaye aliishi miaka 400 kabla ya Torati ya Musa kutolewa, alivyookolewa kwa imani. Alionesha kwamba kama vile Torati haingeweza kumwokoa mtu, basi hakuna mtu angeweza kuwa mkamilifu kwa kujitahidi kwa uwezo wake mwenyewe kuitimiza Torati.MwandishiMtume Paulo.KusudiKukataa mafundisho ya kuwa muumini wa Mataifa ni lazima atii Torati ndio aokolewe.MahaliAntiokia.TareheMnamo 49 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Tito, Barnaba, Petro, na walimu wa uongo.Wazo KuuPaulo anatetea kwa bidii kweli ya Injili ambayo kiini chake ni kwamba, “Mtu anaokolewa kwa neema ya Mwenyezi Mungu kwa kumwamini Al-Masihi.”Mambo MuhimuPaulo anasisitiza uhalali wa Injili, ubora wa Injili, na uhuru wa Injili.YaliyomoPaulo atetea Injili na mamlaka yake kama mtume (1:1–2:21)Kuwekwa huru kutokana na Torati (3:1–4:31)Uhuru wa mfuasi wa Al-Masihi (5:1-26)Mawaidha kuhusu mwenendo wa mfuasi wa Al-Masihi (6:1-18).