Zaburi 110 - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

Zaburi 110Mwenyezi Mungu na mfalme wake mteuleZaburi ya Daudi.

1Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

hadi nitakapowafanya adui zako

kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”

2Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;

utatawala katikati ya adui zako.

3Askari wako watajitolea kwa hiari

katika siku yako ya vita.

Ukiwa umevikwa fahari takatifu,

kutoka tumbo la mapambazuko

utapokea umande wa ujana wako.

4Mwenyezi Mungu ameapa,

naye hatabadilisha mawazo yake:

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

5Bwana yuko mkono wako wa kuume,

atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

6Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga

na kuwaponda watawala wa dunia nzima.

7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia;

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help