2 Wakorintho Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziIngawa inaonekana kwamba waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wakorintho uliwasaidia, bado mivutano na mashindano yalikuwa yakiendelea. Walimu wa uongo walikuwa wamejiingiza ndani ya kundi la waumini, wakiwa wanapinga na hata kushambulia uadilifu wa Paulo mwenyewe, na mamlaka yake kama mtume. Wengine katika kundi la waumini hawakutaka kutubu. Hivyo Paulo aliamua kutorudi huko hadi tabia zao zibadilike.Paulo aliandika waraka huu kueleza hisia zake kuhusu wajibu, shauku na majukumu katika ushirika wa Wakorintho, na pia kujibu mashambulizi yaliyokuwa yameelekezwa kwake binafsi kama mtume. Katika kushughulikia matatizo hayo, Paulo alithibitisha mamlaka yake kama mtume.MwandishiMtume Paulo.KusudiKuthibitisha huduma ya Paulo, na kutetea uwezo wake kama mtume, na pia kuyakataa mafundisho ya uongo katika kundi la waumini la Korintho.MahaliMakedonia.TareheMnamo 55–57 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Tito, Timotheo, na walimu wa uongo.Wazo KuuMaisha binafsi na utumishi wa Paulo: anaorodhesha mambo aliyoyapitia katika maisha yake kama mtumishi wa Al-Masihi.Mambo MuhimuJinsi tunavyoweza kupata ushindi katika mateso, na jinsi neema ya Mwenyezi Mungu inavyotenda kazi kuleta mema kutokana na mateso. Paulo pia anatetea utume wake na kuwaonya wasiotii.YaliyomoSalamu na utambulisho, faraja kwa wafuasi wa Al-Masihi (1:1–2:17)Maelekezo kuhusu huduma ya kweli (3:1–6:2)Habari za Paulo mwenyewe (6:3–7:16)Neema ya utoaji na maelekezo kuhusu changizo (8:1–9:15)Utetezi wa Paulo kuhusu huduma yake (10:1–12:21)Maonyo ya mwisho, na salamu (13:1-14).