Habakuki Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziJina “Habakuki” maana yake ni “Kumbatia”. Habakuki alikuwa nabii wa Yuda kutoka kabila la Lawi na alikuwa mmoja wa waimbaji katika Hekalu. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo wa mazungumzo kati ya Mwenyezi Mungu na nabii. Habakuki hakuelewa jinsi gani Mwenyezi Mungu angeweza kuwatumia Wakaldayo, waliokuwa waovu kuliko Wayahudi, kutekeleza hukumu dhidi ya watu waliokuwa wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu. Jibu la Mwenyezi Mungu lilikuwa kwamba wenye haki wangeishi kwa imani. Mwenyezi Mungu alimwambia Habakuki kwamba bila kukawia, Wakaldayo wangehukumiwa na haki ingetawala kwa ajili ya watu wa Mwenyezi Mungu.MwandishiHabakuki.KusudiKuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu anatawala dunia na atahukumu kila uovu kwa wakati wake, na kwamba mwenye haki ataishi kwa imani.MahaliYuda.TareheMnamo 612–589 K.K.Wahusika WakuuHabakuki, na Wakaldayo.Wazo KuuMwenye haki ataishi kwa imani.Mambo MuhimuMwenyezi Mungu hutumia watu waovu kuwaadhibu watu wake wanapomwasi. Lengo ni kuwarejesha katika uhusiano mwema naye. Hivyo, wenye haki wanapaswa kuishi kwa imani wakijua kuwa Mwenyezi Mungu ana mamlaka na haki ya kutumia njia aitakayo kuwaadhibu wakosaji.YaliyomoSwali la Habakuki na jibu la Mwenyezi Mungu (1:1-11)Swali la pili la Habakuki na jibu la Mwenyezi Mungu (1:12–2:20)Maombi ya Habakuki (3:1-19).