Ruthu Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024

UtanguliziKitabu hiki kimepewa jina la Ruthu, mhusika mkuu katika habari zilizoandikwa humu. Elimeleki na mkewe Naomi walilazimika kuhama kutoka Bethlehemu kwenda nchi ya Moabu. Muda mfupi baadaye, Elimeleki akafariki, nao wanawe Maloni na Kilioni wakaoa wanawake wa Kimoabu, Ruthu na Orpa. Maloni na Kilioni wakafariki bila watoto. Naomi alipoamua kurudi nyumbani mwake katika nchi ya Yuda, aliwashawishi wakwe wake kurudi kwao. Ruthu alisisitiza kwenda naye, lakini Orpa aliamua kurudi nyumbani.Naomi na Ruthu walipofika Israeli, Ruthu alienda kutafuta riziki yao. Alijikuta katika mashamba ya mtu wa jamaa wa karibu wa Elimeleki, kwa jina Boazi, ambaye aliamuru Ruthu atunzwe na wafanyakazi wake. Baada ya muda, Boazi alimwoa Ruthu. Ukoo wa ufalme wa Israeli ulioanza na Mfalme Daudi ulitoka kwa ukoo huu. Baadaye Masihi, Isa Al-Masihi, anatajwa kuwa wa ukoo huu.MwandishiHajulikani, lakini mapokeo ya Kiyahudi yanasema Samweli ndiye mwandishi.KusudiKitabu cha Ruthu kinaonesha jinsi watu watatu wanaweza kuwa na mwenendo thabiti na wa uadilifu kwa Mwenyezi Mungu wakati jamii inayowazunguka imepotoka.MahaliMoabu na Bethlehemu.TareheBaada ya kipindi cha Waamuzi, kama 1050 K.K.Wahusika WakuuNaomi, Ruthu na Boazi.Wazo KuuUhusiano kati ya Naomi na mkwewe Ruthu unatupatia kielelezo jinsi maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu yanavyopaswa kuwa, na vile upendo wa kweli kwa jirani unavyoweza kuwa na matokeo ya baraka.Mambo MuhimuKuambatana kwa Ruthu na Naomi kunaonesha uaminifu wa Ruthu, ijapokuwa Naomi alimsihi arudi kwa watu wake baada ya kufiwa na mumewe. Kutokana na uaminifu huo, Ruthu anatajwa katika uzao wa Isa kutokana na kuolewa na Boazi.YaliyomoNaomi kuondoka Israeli, na kurudi kwake na Ruthu (1:1-22)Ruthu anakaribishwa (2:1-23)Ruthu na Boazi (3:1–4:22).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help