Marko Utangulizi - Kiswahili Contemporary Scriptures 2024
UtanguliziYohana Marko, mwandishi wa Injili hii, alitajwa na mababa wa Jumuiya ya kwanza ya waumini wa Isa, yaani Papiasi, Irenio na Klementi wa Iskanderia, kuwa mshirika wa karibu sana wa Mtume Petro. Yohana Marko alikuwa mtoto wa Mariamu, ambaye nyumba yake ilikuwa kituo kikuu cha Jumuiya ya waumini wa Isa huko Yerusalemu. Hatimaye Marko aliishi Rumi ambako aliandika kumbukumbu za Mtume Petro.Marko alisafiri na mjomba wake, Barnaba, hadi Antiokia ya Siria walipofuatana na Paulo kwenye safari yake ya kwanza kueneza Injili. Hata hivyo, Marko aliwaacha Barnaba na Paulo huko Kipro na kurudi Yerusalemu. Baadaye Barnaba na Marko walielekea Kipro wakati Paulo alienda jimbo la Asia. Miaka kama kumi baadaye, Marko alikuwa pamoja na Paulo huko Rumi. Shabaha ya Marko ilikuwa kukusanya pamoja ujumbe wote wa Injili ya Al-Masihi kwa kifupi.MwandishiYohana Marko.KusudiKumtambulisha Isa, kazi, na mafundisho yake.MahaliRumi.TareheMnamo 55–65 B.K.Wahusika WakuuIsa Al-Masihi na wanafunzi wake, Pilato, na viongozi wa dini ya Kiyahudi.Wazo KuuMarko anamdhihirisha Bwana Isa kuwa Mtumishi wa Mwenyezi Mungu, na Mtu wa vitendo aliyekuja kuyatimiza mapenzi ya Mwenyezi Mungu.Mambo MuhimuMarko anaanza kwa kueleza habari za huduma ya Bwana Isa hadharani na mahubiri yake kuhusu Habari Njema za ufalme wa Mwenyezi Mungu. Kisha anatoa wazi unabii kuhusu matazamio ya kifo cha Bwana Isa. Hatimaye anaeleza jinsi Bwana Isa alivyosulubiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na alivyofufuliwa kutoka kwa wafu; pia maneno na maagizo yake ya mwisho kwa wanafunzi wake.YaliyomoHuduma ya Yahya (1:1-13)Huduma ya Isa huko Galilaya (1:14–9:50)Safari ya kwenda Yerusalemu na matukio mjini (10:1–12:44)Unabii kuhusu mambo yajayo (13:1-37)Kufa na kufufuka kwa Isa (14:1–16:20).