1Msifuni Mwenyezi Mungu.
Enyi watumishi wa Mwenyezi Mungu msifuni,
lisifuni jina la Mwenyezi Mungu.
2Jina la Mwenyezi Mungu na lisifiwe,
sasa na hata milele.
3Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,
jina la Mwenyezi Mungu linapaswa kusifiwa.
4Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya mataifa yote,
utukufu wake juu ya mbingu.
5Ni nani aliye kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,
Yule aliyeketi kwenye kiti cha enzi huko juu,
6ambaye huinama atazame chini
aone mbingu na nchi?
7Huwainua maskini kutoka mavumbini,
na kuwanyanyua wahitaji
kutoka lundo la majivu,
8huwaketisha pamoja na wakuu,
pamoja na wakuu wa watu wake.
9Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,
akiwa mama watoto mwenye furaha.
Msifuni Mwenyezi Mungu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.