3 Yohana Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziWaraka wa tatu wa Yohana uliandikiwa Gayo, ambaye alikuwa kiongozi muhimu katika kanisa. Alielekezwa kuwasaidia na kuwahudumia wajumbe wa Mungu waliotembea kanisani. Pia alipewa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano. Yohana alieleza tarajio lake la kuja na kushughulikia tatizo hili mwenyewe.MwandishiMtume Yohana.KusudiYohana anamwandikia Gayo akimpa onyo kuhusu Deotrefe, kwa tabia yake ya kukosa ushirikiano.MahaliEfeso.TareheMnamo 90 B.K.Wahusika WakuuYohana, Gayo, Deotrefe, na Demetrio.Wazo KuuWajibu binafsi wa Gayo kuhusu watumishi wa kweli na wa uongo.Mambo MuhimuYohana anamtakia Gayo kufanikiwa katika mambo yote, na pia anamwagiza asiige lililo baya bali aige lililo jema.YaliyomoSalamu (1‑4)Gayo anatiwa moyo (5‑8)Deotrefe anakemewa (9‑10)Demetrio anasifiwa (11‑12)Hitimisho (13‑15).