Tito Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziTito, kama vile Timotheo, alikuwa mshirika na rafiki wa karibu wa Paulo katika huduma yake. Alikuwa muumini asiyetahiriwa, mtu wa Mataifa kutoka Antiokia. Alifuatana na Paulo na Barnaba kuhudhuria Baraza la Yerusalemu. Paulo alimwandikia Tito waraka huu muda mfupi tu baada ya kumwachia wajibu wa kuliangalia na kuliimarisha kanisa la Krete. Tito alikuwa na wajibu wa kuwateua wazee wa kanisa, kuwaweka wakfu, na kuwafundisha kushika misingi ya imani ya Kikristo.Waraka huu unaonesha kuwa kanisa la Krete halikuwa na mpangilio mahsusi. Ilimbidi Paulo aeleze kwa kina kuhusu sifa za wazee wa kanisa, na pia kutoa mafundisho kwa waumini. Paulo aligusia matatizo yanayowapata watumishi wa Mungu, na jinsi yanavyoweza kutatuliwa.MwandishiMtume Paulo.KusudiKumshauri Tito kuhusu wajibu wake wa uangalizi wa makanisa katika kisiwa cha Krete.MahaliPengine ni Korintho.TareheMnamo 64 B.K.Wahusika WakuuPaulo na Tito.Wazo KuuIngawa katika maisha yetu hapa duniani tumezungukwa na uovu na chuki, hatuna budi maisha yetu kuwa kielelezo jinsi neema ya Mungu inatupatia ushindi.Mambo MuhimuKuweka mpango na uangalizi wa makanisa, na jinsi ya kufanya kazi hiyo. Mkazo wa barua hii ni kuhusu kuishi maisha matakatifu katika Kristo katikati ya uovu ulioko duniani. Paulo anarudia mara kwa mara kusisitiza kudumisha matendo mema.YaliyomoSalamu, na wajibu wa Tito huko Krete (1:1‑16)Fundisha wote mafundisho manyofu (2:1‑15)Maagizo mbalimbali, na maneno ya mwisho (3:1‑15).