Wakolosai Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziNyaraka za Waefeso na Wakolosai zinaitwa pacha kwa sababu mambo yaliyomo yanafanana. Timotheo alishirikiana na Paulo huko Rumi katika kuandika nyaraka hizi mbili; Wakolosai ni mojawapo ya nyaraka za gerezani. Tikiko ndiye aliupeleka waraka huu Kolosai.Mji wa Kolosai ulikuwa umejengwa kama kilomita 160 kutoka Efeso kwenye Bonde la Lika, karibu na Hierapoli na Laodikia. Kwa kadiri ionekanavyo, Paulo alikuwa hajautembelea mji wa Kolosai, ila mji huu ulihubiriwa Injili na Epafra wakati Paulo alikuwa Efeso. Paulo alipata kuwafahamu waumini hawa akiwa Efeso katika safari yake ya pili kueneza Injili. Sasa alikuwa na wasiwasi kwa sababu alisikia kuwa mafundisho ya Unostiki yalikuwa yameingia katika kanisa hilo. Mafundisho haya yalikuwa yakiuelekeza ujumbe wa Injili hatarini.MwandishiMtume Paulo.KusudiKupinga mafundisho ya uzushi katika kanisa, na kuwaonesha waumini kwamba wana kila kitu wanachokihitaji katika Kristo.MahaliRumi.TareheMnamo 60 B.K.Wahusika WakuuPaulo, Timotheo, Tikiko, Onesimo, Aristarko, Marko, na Epafra.Wazo KuuKuthibitisha utoshelevu wa Kristo, ukilinganishwa na utupu wa filosofia ya mwanadamu.Mambo MuhimuMambo yaliyokuwa yakiwasumbua Wakolosai: Mchanganyiko wa elimu ya nyota, uchawi, na mafundisho ya Unostiki ambayo yalisema kwamba Kristo alikuwa sawa na malaika.YaliyomoSalamu, shukrani na maombi (1:1‑14)Yesu Kristo na waumini (1:15–2:7)Hatari za mafundisho ya uongo (2:8‑23)Mafundisho kuhusu maisha ya Kikristo (3:1–4:1)Maagizo zaidi, na mausia ya mwisho (4:2‑18).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help