Zaburi 46 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 46Mungu yuko pamoja nasiKwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi.

1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

2Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa,

na milima ianguke kilindini cha bahari,

3hata maji yake yakinguruma na kuumuka,

na milima itetemeke kwa mawimbi yake.

4Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu,

mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.

5Mungu yuko katikati yake, hautaanguka,

Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

6Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka,

yeye hupaza sauti yake, dunia ikayeyuka.

7 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi;

Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

8Njooni mkaone kazi za Bwana

jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.

9Anakomesha vita hata miisho ya dunia,

anakata upinde na kuvunjavunja mkuki,

anateketeza ngao kwa moto.

10“Tulieni, mjue kwamba mimi ndimi Mungu;

nitatukuzwa katikati ya mataifa,

nitatukuzwa katika dunia.”

11 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi;

Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help