Yohana Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
UtanguliziMiongoni mwa Injili zote nne, Injili ya Yohana ni ya kipekee. Ingawa kwa ujumla inaonesha maisha ya Yesu na huduma yake, Injili hii haina mifano. Injili ya Yohana inaelezea miujiza saba; kuna miwili iliyonakiliwa katika Injili zile zingine, na miujiza mitano ambayo Yohana peke yake aliielezea.Yohana anaandika jinsi Yesu anavyojidhihirisha kuwa ni Mungu kwa semi saba za “Mimi Ndiye”. Hivi ndivyo Mungu alivyojidhihirisha kwa Waisraeli huko Misri. Kwa hiyo, ni wazi kwamba Yesu ni Yehova.MwandishiYohana mwana wa Zebedayo, nduguye Yakobo.Kusudi“Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake” (20:31).MahaliUwezekano mkubwa ni kwamba Injili hii iliandikiwa Efeso.TareheMnamo 85–90 B.K.Wahusika WakuuYesu, mama yake, na wanafunzi wake Yesu; Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake; Mariamu, Martha na Lazaro; Pilato, wakuu wa dini ya Kiyahudi, na Mariamu Magdalene.Wazo KuuInjili ya Yohana inatilia mkazo zaidi Uungu wa Kristo. Pia inatueleza kwa undani zaidi ishara ambazo Injili zingine zinaziita miujiza, ili msomaji aweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na kwamba mtu anaweza kupata uzima wa milele tu kwa kumwamini Yesu.Mambo MuhimuKatika Injili hii, tunapata habari kuhusu baadhi ya miujiza ya Yesu, na mafundisho yake ambayo hayakutajwa katika Injili zingine. Sehemu ya sura 14–17 inaeleza kwa kina mafundisho ambayo Yesu aliwapa wanafunzi wake kabla ya kifo chake. Sehemu ya mwisho inafafanua jinsi Yesu alivyojidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwake.YaliyomoNeno alifanyika mwili (1:1‑18)Huduma ya Yesu kabla ya kurudi Galilaya (1:19–4:54)Huduma ya Yesu huko Galilaya, na upinzani uliomkabili huko Yerusalemu (5:1–10:42)Yesu amfufua Lazaro (11:1‑57)Yesu akamilisha huduma yake (12:1–13:30)Mafundisho ya mwisho ya Bwana Yesu (13:31–17:26)Kufa na kufufuka kwa Yesu (18:1–20:10)Yesu aonekana baada ya kufufuka (20:11–21:25).