1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana,
macho yangu hayajivuni;
sijishughulishi na mambo makuu kunizidi
wala mambo ya ajabu mno kwangu.
2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,
kama mtoto aliyeachishwa kunyonya
ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu.
3Ee Israeli, mtumaini Bwana
tangu sasa na hata milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.