Hesabu Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziKitabu cha Hesabu kimepewa jina hili kutokana na matukio mawili ya kuwahesabu Waisraeli: La kwanza huko Sinai katika mwaka wa pili baada ya kutoka Misri (Hes 1), na la pili huko Yordani katika mwaka wa arobaini (Hes 26). Jina la kitabu hiki kwa Kiebrania ni “Bemidbar,” ambalo maana yake ni “Huko jangwani,” jina linaloeleza zaidi mambo yaliyomo.Kitabu hiki kinatoa maelezo ya safari ya Waisraeli ya miaka 38 wakati walikuwa wanatangatanga jangwani baada ya kuanzishwa kwa Agano la Mungu katika Mlima Sinai. Kitabu cha Hesabu kinagusia safari ya Waisraeli kutoka Mlima Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu katika mpaka wa Kanaani. Kitabu hiki kinaelezea vile Waisraeli walivyonungʼunika na kumwasi Mungu, na hukumu iliyofuata baadaye. Watu wazima waliotoka Misri walikosa nafasi ya kuingia katika Nchi ya Ahadi, isipokuwa watoto wao.MwandishiMusa.KusudiKuelezea jinsi Waisraeli walivyojitayarisha kuingia katika Nchi ya Ahadi, na walivyoasi na kuhukumiwa.MahaliKitabu hiki kiliandikwa wakati Waisraeli walikuwa wanatangatanga jangwani, mahali fulani katika Ghuba ya Sinai.TareheMnamo 1450–1410 K.K.Wahusika WakuuMusa, Haruni, Miriamu, Yoshua, Kalebu, Eleazari, Kora, Balaamu na Balaki.Wazo KuuKitabu hiki kinaeleza juu ya utunzaji na uongozi wa Mungu, uvumilivu wake, na uasi wa watu wa Mungu na matokeo yake. Jambo moja lililokuwa dhahiri na ambalo limerudiwa mara kwa mara katika kitabu chote ni jinsi mkono wa Mungu ulivyokuwa pamoja na Waisraeli saa zote ili kuwahudumia na kuwapa mahitaji yao.Mambo MuhimuKuhesabiwa kwa Waisraeli, uasi dhidi ya Mungu, na hukumu ya Waisraeli ya kutangatanga jangwani.YaliyomoWatu kuhesabiwa, mpangilio wa kambi, na kuendelea na safari (1:1–10:10)Kutoka Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu, viongozi kuasi Mungu (10:11–21:35)Balaamu, Balaki na Israeli (22:1–25:18)Kuhesabu watu mara ya pili, na Yoshua kuchukua nafasi ya Musa (26:1–27:23)Maagizo mbalimbali (28:1–31:54).Maelekezo kuhusu kuitwaa nchi ya Kanaani (32:1–36:13).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help