Zaburi 137 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 137Maombolezo ya Israeli uhamishoni

1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza

tulipokumbuka Sayuni.

2Kwenye miti ya huko

tulitundika vinubi vyetu,

3kwa maana huko hao waliotuteka

walitaka tuwaimbie nyimbo;

watesi wetu walidai nyimbo za furaha;

walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja

kati ya nyimbo za Sayuni!”

4Tutaimbaje nyimbo za Bwana,

tukiwa nchi ya kigeni?

5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu,

basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.

6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu

kama sitakukumbuka wewe,

kama nisipokufikiri Yerusalemu

kuwa furaha yangu kubwa.

7Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu,

siku ile Yerusalemu ilipoanguka.

Walisema, “Bomoa, bomoa

hata misingi yake!”

8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,

heri yeye atakayekulipiza wewe

kwa yale uliyotutenda sisi:

9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga

na kuwaponda juu ya miamba.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help