Isaya 20 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Unabii dhidi ya Misri na Kushi

1Mwaka ule jemadari mkuu alitumwa na Mfalme Sargoni wa Ashuru, naye akaja Ashdodi, akaushambulia na kuuteka,

2wakati huo Bwana alisema kwa kinywa cha Isaya mwana wa Amozi. Akamwambia, “Vua gunia kutoka mwilini mwako na viatu kutoka miguuni mwako.” Naye akafanya hivyo, akitembea uchi, bila viatu.

3Kisha Bwana akasema, “Kama mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na bila viatu kwa miaka mitatu, kama ishara na dalili mbaya dhidi ya nchi ya Misri na Kushi,

4vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri, na watu wa uhamisho wa Kushi, uchi na bila viatu, vijana hata wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri.

5Wale waliotegemea Kushi na kujivunia Misri wataogopa na kuaibika.

6Katika siku ile watu wanaoishi katika pwani hii watasema, ‘Tazama lililowapata wale tuliowategemea, wale tuliowakimbilia kwa msaada na wokovu kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru! Tutawezaje basi kupona?’ ”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help