Hosea Utangulizi - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

UtanguliziHosea mwana wa Beeri alikuwa mzaliwa wa Ufalme wa Kaskazini, yaani Israeli, ambao pia uliitwa Efraimu. Maana ya jina Hosea ni “Wokovu”. Huduma ya Hosea kwa Ufalme wa Kaskazini ilikaribiana sana na ile ya Amosi. Hawa wawili ndio manabii pekee wa Agano la Kale ambao vitabu vyao vilihusu Ufalme wa Kaskazini na maangamizi yake.Hosea alianza huduma yake miaka ya baadaye ya utawala wa Yeroboamu wa Pili, wakati Israeli ikifurahia utulivu wa kisiasa na ustawi wa kiuchumi. Kufuatia kifo cha Yeroboamu wa Pili mnamo 753 K.K., hali ya taifa la Israeli ilibadilika. Amani na utulivu katika taifa vilitoweka. Taifa likaporomoka na kuangamia. Waisraeli wakapigwa na Waashuru na kisha kupelekwa uhamishoni mnamo 722 K.K.MwandishiHosea.KusudiKuonesha upendo mkuu wa Mungu kwa Waisraeli waliokuwa wamemwasi. Watu wanapomwacha na kumwasi, Mungu anaendelea kuwapenda na kuwarejesha kwake.MahaliUfalme wa Kaskazini yaani Israeli, ambao uliitwa Efraimu.TareheMnamo 715–710 K.K.Wahusika WakuuHosea, Gomeri, na watoto wao.Wazo KuuHukumu na upendo mkuu wa Mungu kwa watu wake.Mambo MuhimuHosea anaelezea hali ya taifa la Israeli akitumia hali iliyojitokeza katika maisha ya kila siku. Mungu anafananishwa na: mume, baba, simba, chui, dubu, umande, mvua, nondo, na mifano mingine. Israeli inafananishwa na: mke aliyekosa uaminifu kwa mumewe, mtu mgonjwa, mzabibu, mzeituni, mwanamke anayejifungua, jiko la kuokea, ukungu wa asubuhi, makapi, moshi, na mifano mingine.YaliyomoMaisha ya Hosea katika jamii (1:1–3:5)Hali ya dhambi ya Israeli (4:1–10:15)Hukumu ya Mungu na rehema zake (11:1–14:9).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help