Zaburi 5 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 5Sala kwa ajili ya ulinzi wakati wa hatariKwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi.

1Ee Bwana, tegea sikio maneno yangu,

uangalie kupiga kite kwangu.

2Sikiliza kilio changu ili unisaidie,

Mfalme wangu na Mungu wangu,

kwa maana kwako ninaomba.

3Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Bwana;

asubuhi naleta haja zangu mbele zako,

na kusubiri kwa matumaini.

4Wewe si Mungu unayefurahia uovu,

kwako mtu mwovu hataishi.

5Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,

unawachukia wote watendao mabaya.

6Unawaangamiza wasemao uongo.

Bwana huwachukia

wanaomwaga damu na wadanganyifu.

7Lakini mimi, kwa rehema zako kuu,

nitakuja katika nyumba yako,

kwa unyenyekevu, nitasujudu

kulielekea Hekalu lako takatifu.

8Niongoze katika haki yako, Ee Bwana,

kwa sababu ya adui zangu,

nyoosha njia yako mbele yangu.

9Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika,

mioyo yao imejaa maangamizi.

Koo lao ni kaburi lililo wazi,

kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.

10Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu!

Hila zao ziwe anguko lao wenyewe.

Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi,

kwa kuwa wamekuasi wewe.

11Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi,

waimbe kwa shangwe daima.

Ueneze ulinzi wako juu yao,

ili wale wanaolipenda jina lako

wapate kukushangilia.

12Kwa hakika, Ee Bwana, unawabariki wenye haki,

unawazunguka kwa wema wako kama ngao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help