Zaburi 2 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 2Mfalme aliyechaguliwa na Mungu

1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,

na makabila ya watu kula njama bure?

2Wafalme wa dunia wanajipanga

na watawala wanajikusanya

dhidi ya Bwana

na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

3Wanasema, “Tuvunje minyororo yao

na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”

4Yeye anayetawala mbinguni hucheka,

Bwana huwadharau.

5Kisha huwakemea katika hasira yake

na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

6“Nimemtawaza Mfalme wangu

juu ya Sayuni,

mlima wangu mtakatifu.”

Ushindi wa mfalme

7Nitatangaza amri ya Bwana:

Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu;

leo mimi nimekuwa Baba yako.

8Niombe, nami nitayafanya mataifa

kuwa urithi wako,

na miisho ya dunia kuwa milki yako.

9Utawapondaponda kwa fimbo ya chuma,

na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”

10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;

mwonyeke, enyi watawala wa dunia.

11Mtumikieni Bwana kwa hofu

na mshangilie kwa kutetemeka.

12Mbusu Mwana, asije akakasirika

nawe ukaangamizwa katika njia yako,

kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.

Heri wote wanaomkimbilia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help