Zaburi 70 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 70Kuomba msaada(Za 40:13‑17)Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.

1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;

Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

2Wale wanaotafuta kuniua,

waaibishwe na kufadhaishwa;

wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,

warudishwe nyuma kwa aibu.

3Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!”

na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.

4Lakini wote wanaokutafuta

washangilie na kukufurahia,

wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme,

“Bwana ni mkuu!”

5Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji;

Ee Mungu, unijie haraka.

Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;

Ee Bwana, usikawie.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help