Zaburi 117 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025
Zaburi 117Sifa za Bwana
1Msifuni Bwana, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
2Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa Bwana unadumu milele.
Msifuni Bwana.