Zaburi 138 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 138Maombi ya shukraniZaburi ya Daudi.

1Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote,

mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako.

2Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,

nami nitalisifu jina lako

kwa ajili ya upendo wako

na uaminifu,

kwa maana umeitukuza ahadi yako

zaidi ya jina lako.

3Nilipoita, ulinijibu;

ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

4Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana,

wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako.

5Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana,

kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.

6Ingawa Bwana yuko juu,

humwangalia mnyonge,

bali mwenye kiburi

yeye anamjua kutokea mbali.

7Nijapopita katikati ya shida,

wewe unayahifadhi maisha yangu,

unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu,

kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.

8 Bwana atatimiza kusudi lake kwangu,

Ee Bwana, upendo wako wadumu milele:

usiziache kazi za mikono yako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help