Zaburi 6 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 6Sala ya kuomba msaada wakati wa taabuKwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,

wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

2Unirehemu Bwana,

kwa maana nimedhoofika;

Ee Bwana, uniponye,

kwa maana mifupa yangu

ina maumivu makali.

3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.

Hadi lini, Ee Bwana, hadi lini?

4Geuka, Ee Bwana, unikomboe,

uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

5Hakuna mtu anayekukumbuka

akiwa amekufa.

Ni nani awezaye kukusifu

akiwa Kuzimu?

6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;

usiku kucha natiririsha

kitanda changu kwa machozi;

nimelowesha kiti changu

kwa machozi yangu.

7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,

yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.

8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,

kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.

9 Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,

Bwana amekubali sala yangu.

10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,

watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help