1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu.
Masikio yako na yawe masikivu
kwa kilio changu unihurumie.
3Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,
Ee Bwana, ni nani angeweza kusimama?
4Lakini kwako kuna msamaha,
kwa hiyo wewe unaogopwa.
5Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
6Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
7Ee Israeli, mtumaini Bwana,
maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli
kutoka dhambi zao zote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.