Zaburi 132 - Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) 2025

Zaburi 132Maskani ya Mungu ya milele huko SayuniWimbo wa kwenda juu.

1Ee Bwana, mkumbuke Daudi

na taabu zote alizozistahimili.

2Aliapa kiapo kwa Bwana

na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:

3“Sitaingia nyumbani mwangu

au kwenda kitandani mwangu:

4sitaruhusu usingizi katika macho yangu,

wala kope zangu kusinzia,

5hadi nitakapompatia Bwana mahali,

makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

6Tulisikia habari hii huko Efrata,

tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:

7“Twendeni kwenye makao yake,

na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;

8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia,

wewe na Sanduku la nguvu zako.

9Makuhani wako na wavikwe haki,

watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”

10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako,

usimkatae mpakwa mafuta wako.

11 Bwana alimwapia Daudi kiapo,

kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:

“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe

kwenye kiti chako cha ufalme,

12kama wanao watashika agano langu

na sheria ninazowafundisha,

ndipo wana wao watakalia kiti chako cha ufalme

milele na milele.”

13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni,

amepaonea shauku pawe maskani yake:

14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele;

hapa ndipo nitakapoketi nikitawala,

kwa sababu nimepaonea shauku:

15Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele:

nitashibisha maskini wake kwa chakula.

16Nitawavika makuhani wake wokovu,

nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.

17“Hapa nitamchipushia Daudi pembe,

na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu.

18Adui zake nitawavika aibu,

bali taji kichwani pake litangʼaa sana.”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help