1Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,
“Twende nyumbani mwa Bwana.”
2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama
malangoni mwako.
3Yerusalemu imejengwa vyema kama mji
ulioshikamana pamoja.
4Huko ndiko makabila hukwea,
makabila ya Bwana,
kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo
waliopewa Israeli.
5Huko viti vya hukumu hukaa,
viti vya ufalme vya nyumba ya Daudi.
6Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:
“Wote wanaokupenda na wawe salama.
7Amani na iwe ndani ya kuta zako,
na usalama ndani ya ngome zako.”
8Kwa ajili ya ndugu na rafiki zangu,
nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
9Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu,
nitatafuta mafanikio yako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.